SEMA NA ARTISTS!

Monday, August 30, 2010

So Pwaa by Cpwaa ( New) - Full Video

Friday, August 27, 2010

Cpwaa new Video and Song: Preview

Saturday, August 21, 2010

Kikwete2010 Official Website



Tembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 upate habari mbalimbali kama:

• Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.
• Mafanikio katika sekta mbalimbali.
• Sera na Malengo 2010 – 2015.
• Ratiba za kampeni.
• Hotuba maalumu.
• Matoleo ya Habari.
• Video na picha.
• Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.

Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.

“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”

Friday, August 20, 2010

My Fiesta performance last year with Busta Rhymes


Wednesday, August 18, 2010

Usanii kwa Wasanii????

WASANII WALIOUZIWA VIWANJA MKURANGA WAMETAPELIWA

Asasi moja inayojitambulisha kuwa inashughulikia wasanii,inadaiwa kutapeliwa mashamba waliyodai kuyanunua katika kijiji cha Mwanzega,wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa ajili ya Waandishi wa habari na wasanii.

Uongozi wa Serikali ya ya wilaya ya Mkuranga,umetoa maelezo kuwa,wale wote waliouziwa mashamba hayo wametapeliwa,kwani si mamlaka za wilaya wala Halmashauri zilizohusika kwa namna yoyote ile katika mchakato huo.Mkuu wa wilaya hiyo,Henry Clemence,amesema tayari jeshi la polisi wilayani humo limeingilia kati na kuwashikilia kwa muda Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wa asasi hiyo (jina tunalo).

Alisema kuwa hadi sasa,Mtendaji wa kijiji hicho hajulikani alipo baada ya kutoroka,kwa kujua kuwa anasakwa na vyombo vya dola.

Clemence alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na Nipashe,baada ya watu waliochukuliwa fedha kupitia taasisi hiyo kutua wilayani humo kwa lengo la kukabidhiwa ‘MAENEO YAO’. “Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo,wilaya hii ipo karibu na jiji la dare s salaam..inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga.

Kwa wanaotaka kuja huku (Mkuranga),nawashauri wafuate taratibu,wasivunje amani iliyopo…wanaotaka ardhi wapitie Halmashauri,wasipitie katika asasi wala kwa mtu yeyote kwa sababu taratibu za kumiliki aradhi hazielekezi hivyo,”alisema mkuu huyo.

Monday, August 16, 2010

Things you dont know about me...Cpwaa!

  1. Real name Ilunga Khalifa Born in 1982, March 2nd, mtoto wa kipekee wa Sophia Ali na Khalifa Juma.Mama Msukuma, Baba Mrangi.
  2. Nilianza mziki toka mwaka 1995 nikiwa naimba kwa lugha ya kiingereza tuu! My biggest role model then were Kriss kross, N.W.A, Cypress Hill, Guru, Wu-Tang Clan, House of Pain,MC Hammer, Michael Jackson, Vanilla Ice,Shaba ranks, Sade,Salt n paper,Tribe called Quest,Nas, Jeru da maja, and Boot Camp click .
  3. Nilikuwa bingwa wa Rap kanda ya kusini mwaka 1999 nikashinda zawadi ya TSH 30,000 pale ukumbi wa NBC Mbeya chini ya TBL. Balozi wa Sprite na Cowbell milk mwaka 1998-1999 Mbeya.
  4. Nilimaliza na kufaulu Mbeya secondary School ( Mbeya day) kwa division 1. Mwaka 1999 kutoka darasa la Science 1.
  5. Nilichaguliwa shule moja aliyomaliza Rais wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa, kigonsera High school, Mbinga songea.Nikasoma form 5 tuu kabla ya kuhamishwa Pugu Secondary ambako nilikataa na kuhamia Benjamin William Mkapa ( City High School) sababu ya ubushi wa mjini. I was not a boarding school kid! I loved free life!
  6. Nilijiunga na kundi la NEW JACK FAMILY 2001,kariakoo na kina Dully Sykes,Abby SKillz, Marehemu Complex,Queen Doreen, Gorilla killers,A-Tu, na Zaharani kabla ya kujiunga PARK LANE na Suma Lee 2002 huko Tanga.
  7. Miaka yangu yote toka form 2 nafuga nakusuka nywele, nishagombana sana na uongozi wa shule kuhusu hilo.Nilikata nywele zangu form 4 kabla ya graduation na form 5 kigonsera baada ya mkuu wa shule kusema sipati uhamisho mpaka nikate nywele. I believe in self confidence and freedom of choice.
  8. Miaka yangu yote shule toka Primary school, niko ndani ya top 5 nikiporomoka top 10 na nilikuwa siiingi vipindi vingi darasani especially chuo nilipokuwa,niko busy na tours za muziki lakini matokeo yakitoka ni " A A A" uliza niliosoma nao.
  9. Nilikuwa mwanachuo/ Msanii pekee niliyegraduate na msuko IFM mwaka 2006 ( IFM Class of 2003- 2006)mwenye stashahada ya ICT.
  10. Nilikuwa na bado ni mwanachama wa studio kubwa Tanzania, Bongo records.
  11. Nilipata na bado nafanya kazi kwenye one of the first and still leading Tanzania High Tech Companys . www.6telecoms.co.tz and www.push.co.tz immediately after college.
  12. Msanii wa kwanza kuzindua music video ( 6 in the morning), Slip Way little theatre 1996, nakualika wadau kibao wa muziki Salama Jabri, Gadner, Channel 10, Prime Times na waandishi wa habari kibao.
  13. Moja ya wasanii wachanga waliowahi kuanza game kitambo na kuimba stage moja na KBC wa kwanza Unit, Balozi na Saigon wa Diplomats,Solo Thang na Wateule, Mac D, Mr. II, Soggy Doggy Anter, GWM, Adili wa Chapakazi,na Jay Moo toka miaka ya 90.
  14. Msanii mwenye kipaji cha hali ya juu kwenye uchoraji wa penseli,rangi za maji na mafuta na ubunifu wa kutathmini kupitia picha za kupiga. A+ form 4 n 6 kwenye Fine Arts na uigizaji.
  15. Nimeshashirikiswa kwenye album ya Wanaume family kabla hawajatengana album ya mwisho nyimbo inaitwa " Live bila Chenga" chini ya PFUNK majani, pamoja na album ya Bongo records mwaka 2006-2007.
  16. Msanii aliyeanzisha na kutambulisha muziki wa CRUNK mwaka 2006 akiwa na producer lucci, Afrika ya Mashariki na mpaka leo wananiita KING of BONGO CRUNK.
  17. Nishawahi kupokea kichapo kutoka kw PINA wa KIKOSI CHA MIZINGA ( sababu=Confidential) na leo ni washkaji na tunaishi sehemu moja, Block 41.
  18. Msanii wa kwanza Tanzania kufanya Uzinduzi mdogo na kuvunja rekodi ya mauzo ya vinywaji kwenye FIVE STAR HOTEL Tanzania, Movenpic mwaka 2009 Desemba ( Cpwaa Pre-Launch party).
  19. Msanii wa kwanza Tanzania kuanzisha blogspot kwa kutumia njia tofauti mpaka leo: simu ya mikononi: http://www.simuyangukamera.blogspot.com
  20. Msanii mwenye tuzo ya Kili Music award, video bora ya mwaka 2009.
  21. Msanii wa Bongo anayependwa zaidi na wanafunzi wa Primary, Secondary,International Schools, na Vyuoni, kuanzia umri wa miaka 13 mpaka 29. according to BABKUBWA MAGAZINE, EATV SKONGA na CLOUDS FM XXL SHOW.
  22. Japo wananiita king of Bongo Crunk, Cpwaa ni shabiki mkubwa na mchezaji mzuri wa miziki ya DanceHall, House na Bolingo.
  23. Wasanii wa muziki wa dance haswa Bolingo humfananisha na kumuona mwenzao kutokana na muonekano wake na jina lake " ILUNGA" ambalo pia ni maarufu kule na watu wa CONGO.
  24. CP alipewa jina la CPWAA na Msanii mwenzake Mr. Blue akiwa chini ya Mkurugenzi wake Gadner G. Habash mwaka 2006 na mpaka leo limekuwa popular zaidi kuliko CP.
  25. Napenda sana kula Sea Food,Movies, Kusafiri, Science fictions, Animals programs, Techo updates,Cartoons and i love my drink sessions.
So what's the point on all this? Just incase you find it non sense:

Skip the post and pretend you didn't read this or " Keep yours eyes close to CPWAA, because he is the next Big Thing "

visit my official website for more concrete info www.cpwaa.co.tz

Pwaaaaaa!


Things you didn't know about Cpwaa!

Hapo ni my Caring Father ( Mr.Khalifa) me and my My Lovely God Mother ( Sophia) at IFM ( Institute of Finance Management) 2006 Hapo is when i graduated with degree in IT.

Graduation ya form 4, kipindi mi niko form 3 mwaka 1998. Nikashusha bonge la ngoma inaitwa "Bye bye" na "Pull up your socks"

Maigizo ( Ukimwi na vijana), graduation darasa la 7, Azimio Primary School hapo ukumbi wa mesi Mbeya hospital 1995. put me on the movie now, i still got it, i was born with it.

That's is how it all started! Mwaka 1996 Club Valentino pale Green Belt Hotel,Uhindini Mbeya ilikuwa party yetu ya welcome form 1, hapo nachana ngeli tu CD bado zilikuwa hazijasambaa mwendo wa tape, beat ni za mamtoni.

To see more photos of me since waaaays back in the game visit my facebook profile, make sure upo facebook:

http://www.facebook.com/?ref=home#!/album.php?aid=55459&id=1460884857







Friday, August 13, 2010

Mradi wa kijiji cha Wasanii


Katika kutimiza mpango mzima wa KILIMO KWANZA serikali yetu imegawa maeneo maalumu kwa wanachi ili kuyaendeleza. kupitia shirikisho la wasanii Tanzania ( SHIWATA), Serikali imegawa mahekari kibao kwa wasanii, wanamichezo na wadau wa sanaa nchini huko maeneo ya Mkulanga, Visegese DSM bureee!!! ukilima,ukijenga shauri yako!! Personally nampongeza JK kwa hatua hii ya kuzidi kutufikiria wasanii wa TZ.
Hapo nikiwa nishakamata kadi yangu ya wanachama wa SHIWATA pembeni yangu mtangazaji wa Clouds TV na Redio, Zamaradi tukiwa kwenye hatua za mwisho za kupokea hati zetu za viwanja hivyo. Mradi huu ni kwa wasanii woooteee.

B12 wa XXL, Clouds FM naye aliwahi kujiandikisha tukapangiwa plot za karibu...future neighbors.

Chuo cha ualimu Splendid palipo na ofisi za SHIWATA, Ilala bungoni.

Shadei a.k.a Vuvuzela from Clouds TV naye alikuwepo na swaumu kaliii.



Tuesday, August 10, 2010

Safari ya Mbeya kwenye show ya sikukuu ya Nane nane.

Tarehe 7 mwezi August nilifunga safari kuelekea mkoa wa Mbeya ambako nilikuwa nina mwaliko wa kufanya show kwenye sikukuu ya wakulima Nane nane. safari ilichelewa kidogo na tuliondoka Dar mida ya saa 6 mchana hivi. Njia nzima nililala nikaja kushtuka tuko Mo-Town, Morogoro.

Tulikuwa na gari ndogo hivyo safari ilikuwa safiii tu.

Tukatupia lunch pale karibu na Msamvu, stendi ya morogoro. Hapo nikiwa na Sister Lisa ambaye ni moja ya wawakilishi wa kampuni iliyonipa mchongo wa show hiyo Mbeya.

Kabla ya kuendelea na Safari tulipita nyumbani kwa dereva wetu pale Moro kusalimia. Kwao kuna kiwanda cha kutengenezea keki. Hizi keki tunazokula kila siku madukani na stendi kwa sh mia mia. sema sasa hapa zinatengenezwa in a special way alafu za ukweli. Hapo juu jamaa akiweka ile mix/ ingredients kwenye vikombe baaada ya kuchanganywa.

Oveni asilia ya kupikia keki.

Kitu kikiiva kinafanyiwa package, mtu mzima nikitest kiwango.....Tamu usipime.

Ujumbe.

Kupita pande zile za mikumi nikaona baadhi ya wanyama wakiwemo swala.
Hata twiga niliwafumania.



At last baada ya masaa 12 barabarani, tumefanikiwa kupata hoteli kwa zali maana mji mzima hoteli zimejaa kutokana na nane nane. Hapo hata sikuoga na baridi lile, straaight under the blanket.
Mbeya Paradise Inn, maeneo ya Soweto ndio tulipobahatika kulaza ubavu.



Cpwaa ndani ya Nane Nane Mbeya under courtesy of Zain

Asubuhi nikaamkia uwanja wa nane nane kucheki mpango mzima kwa ajili ya show ya baadae. kwenye eneo la Zain ndio ntafanya makamuzi maana wao ndio walinileta Mbeya kwa shughuli hii.

Hapo nilikutana na mdau wa kupiga picha, " Jose" huyu jamaa hakuna mtu asiyemjua Mbeya. Toka nasoma Mbeya day form 1 jamaa ndio alikuwa akitupiga picha mpaka leo anaendeleza libeneke. Mbishi.
Stage nitakayoitumia ikiwa kwenye initial preparation.





Nane 8, Sikukuu ya wakulima - Mbeya

Baada ya kucheki cheki sehemu nitakayopanda baadae na music system, nikaamua kupiga tour kwenye mabanda ya maonyesho. kauli mbiu mwaka huu nane nane ilikuwa " KILIMO KWANZA, MAPINDUZI YA KIJANI, UHAKIKA WA CHAKULA NA KIPATO"


Wazee wa bia, ngano hiyo.






Mbuzi wa maziwa.
Kitimoto.

Giant Cassava! Duh hebu cheki huo muhogo hapo juu ya gari!





Banda la ngozi na bidhaa zake.


Mashine ya kulimia au kupanda mpunga hivi.





Walking down the Mbeya memory lane

Mlima Mbeya, nishapanda sana huo enzi za Primary tulikuwa tukienda picnic.

Mbeya Secondary School, hapo ndio mtu mzima nilipochomoka na divison 1. Hapa ndio Crazy Power mnaemuita Cpwaa siku hizi alipoanza utundu wake. Bahati mbaya ilikuwa jumapili hamna mtu mlinzi akabana nisiingie kupiga picha za ukumbusho.
Kwa watani wetu wa Jadi.




Ukumbi na benki ya NBC, japo nimekuta pamechoka kidogo back in the days hapo ilikuwa soo, mtu mzima ndio nilichukuaga ubingwa wa Rap mkoa wa Mbeya 1999.
Centre /Mbeya Flames or Kwa Masister, this where i played BasketBall sana mpaka pale mziki uliponiteka.




Azimio Primary School, that was my school, not so many changes since i left.This was one of the best, i hope it still is.
Msikiti huu nimeswali sanaaa, uko karibu home pale maeneo ya Bus stand.







Magorofa ya Soko matola a.k.a mabanda ya njiwa a.k.a Brooklyn Flats as i used to call them. Hapo ndio mambo yote yalipoanzia, nimelelewa hapo na Baba yangu toka 1991 -1999. I used to run the Block, sasa watu karibu wote washasepa niliokuwa nao.

Bata la Mbeya na washkaji


Nikienda Mbeya nitafanya kila kitu ila lazima nipite hili kontena la Bar 2000 pale maeneo ya Uhindini, kiota hichi hakichachi, kipo live mpaka usiku wa manane.

Website counter