SEMA NA ARTISTS!

Monday, August 16, 2010

Things you dont know about me...Cpwaa!

  1. Real name Ilunga Khalifa Born in 1982, March 2nd, mtoto wa kipekee wa Sophia Ali na Khalifa Juma.Mama Msukuma, Baba Mrangi.
  2. Nilianza mziki toka mwaka 1995 nikiwa naimba kwa lugha ya kiingereza tuu! My biggest role model then were Kriss kross, N.W.A, Cypress Hill, Guru, Wu-Tang Clan, House of Pain,MC Hammer, Michael Jackson, Vanilla Ice,Shaba ranks, Sade,Salt n paper,Tribe called Quest,Nas, Jeru da maja, and Boot Camp click .
  3. Nilikuwa bingwa wa Rap kanda ya kusini mwaka 1999 nikashinda zawadi ya TSH 30,000 pale ukumbi wa NBC Mbeya chini ya TBL. Balozi wa Sprite na Cowbell milk mwaka 1998-1999 Mbeya.
  4. Nilimaliza na kufaulu Mbeya secondary School ( Mbeya day) kwa division 1. Mwaka 1999 kutoka darasa la Science 1.
  5. Nilichaguliwa shule moja aliyomaliza Rais wa awamu ya tatu Mh.Benjamin Mkapa, kigonsera High school, Mbinga songea.Nikasoma form 5 tuu kabla ya kuhamishwa Pugu Secondary ambako nilikataa na kuhamia Benjamin William Mkapa ( City High School) sababu ya ubushi wa mjini. I was not a boarding school kid! I loved free life!
  6. Nilijiunga na kundi la NEW JACK FAMILY 2001,kariakoo na kina Dully Sykes,Abby SKillz, Marehemu Complex,Queen Doreen, Gorilla killers,A-Tu, na Zaharani kabla ya kujiunga PARK LANE na Suma Lee 2002 huko Tanga.
  7. Miaka yangu yote toka form 2 nafuga nakusuka nywele, nishagombana sana na uongozi wa shule kuhusu hilo.Nilikata nywele zangu form 4 kabla ya graduation na form 5 kigonsera baada ya mkuu wa shule kusema sipati uhamisho mpaka nikate nywele. I believe in self confidence and freedom of choice.
  8. Miaka yangu yote shule toka Primary school, niko ndani ya top 5 nikiporomoka top 10 na nilikuwa siiingi vipindi vingi darasani especially chuo nilipokuwa,niko busy na tours za muziki lakini matokeo yakitoka ni " A A A" uliza niliosoma nao.
  9. Nilikuwa mwanachuo/ Msanii pekee niliyegraduate na msuko IFM mwaka 2006 ( IFM Class of 2003- 2006)mwenye stashahada ya ICT.
  10. Nilikuwa na bado ni mwanachama wa studio kubwa Tanzania, Bongo records.
  11. Nilipata na bado nafanya kazi kwenye one of the first and still leading Tanzania High Tech Companys . www.6telecoms.co.tz and www.push.co.tz immediately after college.
  12. Msanii wa kwanza kuzindua music video ( 6 in the morning), Slip Way little theatre 1996, nakualika wadau kibao wa muziki Salama Jabri, Gadner, Channel 10, Prime Times na waandishi wa habari kibao.
  13. Moja ya wasanii wachanga waliowahi kuanza game kitambo na kuimba stage moja na KBC wa kwanza Unit, Balozi na Saigon wa Diplomats,Solo Thang na Wateule, Mac D, Mr. II, Soggy Doggy Anter, GWM, Adili wa Chapakazi,na Jay Moo toka miaka ya 90.
  14. Msanii mwenye kipaji cha hali ya juu kwenye uchoraji wa penseli,rangi za maji na mafuta na ubunifu wa kutathmini kupitia picha za kupiga. A+ form 4 n 6 kwenye Fine Arts na uigizaji.
  15. Nimeshashirikiswa kwenye album ya Wanaume family kabla hawajatengana album ya mwisho nyimbo inaitwa " Live bila Chenga" chini ya PFUNK majani, pamoja na album ya Bongo records mwaka 2006-2007.
  16. Msanii aliyeanzisha na kutambulisha muziki wa CRUNK mwaka 2006 akiwa na producer lucci, Afrika ya Mashariki na mpaka leo wananiita KING of BONGO CRUNK.
  17. Nishawahi kupokea kichapo kutoka kw PINA wa KIKOSI CHA MIZINGA ( sababu=Confidential) na leo ni washkaji na tunaishi sehemu moja, Block 41.
  18. Msanii wa kwanza Tanzania kufanya Uzinduzi mdogo na kuvunja rekodi ya mauzo ya vinywaji kwenye FIVE STAR HOTEL Tanzania, Movenpic mwaka 2009 Desemba ( Cpwaa Pre-Launch party).
  19. Msanii wa kwanza Tanzania kuanzisha blogspot kwa kutumia njia tofauti mpaka leo: simu ya mikononi: http://www.simuyangukamera.blogspot.com
  20. Msanii mwenye tuzo ya Kili Music award, video bora ya mwaka 2009.
  21. Msanii wa Bongo anayependwa zaidi na wanafunzi wa Primary, Secondary,International Schools, na Vyuoni, kuanzia umri wa miaka 13 mpaka 29. according to BABKUBWA MAGAZINE, EATV SKONGA na CLOUDS FM XXL SHOW.
  22. Japo wananiita king of Bongo Crunk, Cpwaa ni shabiki mkubwa na mchezaji mzuri wa miziki ya DanceHall, House na Bolingo.
  23. Wasanii wa muziki wa dance haswa Bolingo humfananisha na kumuona mwenzao kutokana na muonekano wake na jina lake " ILUNGA" ambalo pia ni maarufu kule na watu wa CONGO.
  24. CP alipewa jina la CPWAA na Msanii mwenzake Mr. Blue akiwa chini ya Mkurugenzi wake Gadner G. Habash mwaka 2006 na mpaka leo limekuwa popular zaidi kuliko CP.
  25. Napenda sana kula Sea Food,Movies, Kusafiri, Science fictions, Animals programs, Techo updates,Cartoons and i love my drink sessions.
So what's the point on all this? Just incase you find it non sense:

Skip the post and pretend you didn't read this or " Keep yours eyes close to CPWAA, because he is the next Big Thing "

visit my official website for more concrete info www.cpwaa.co.tz

Pwaaaaaa!


2 comments:

Anonymous said...

Nyc story mayne, i wish i could b open like u dah!
Cjakosea kusema u r my Role Model!
Deuces(peace n love)!

brill D Lastborn

Anonymous said...

Dah! Nimekukubali mzeiya. We mkali!

Website counter