WASANII WALIOUZIWA VIWANJA MKURANGA WAMETAPELIWA
Asasi moja inayojitambulisha kuwa inashughulikia wasanii,inadaiwa kutapeliwa mashamba waliyodai kuyanunua katika kijiji cha Mwanzega,wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani kwa ajili ya Waandishi wa habari na wasanii.
Uongozi wa Serikali ya ya wilaya ya Mkuranga,umetoa maelezo kuwa,wale wote waliouziwa mashamba hayo wametapeliwa,kwani si mamlaka za wilaya wala Halmashauri zilizohusika kwa namna yoyote ile katika mchakato huo.Mkuu wa wilaya hiyo,Henry Clemence,amesema tayari jeshi la polisi wilayani humo limeingilia kati na kuwashikilia kwa muda Mwenyekiti wa Kijiji hicho pamoja na viongozi wa asasi hiyo (jina tunalo).
Alisema kuwa hadi sasa,Mtendaji wa kijiji hicho hajulikani alipo baada ya kutoroka,kwa kujua kuwa anasakwa na vyombo vya dola.
Clemence alitoa maelezo hayo wakati akizungumza na Nipashe,baada ya watu waliochukuliwa fedha kupitia taasisi hiyo kutua wilayani humo kwa lengo la kukabidhiwa ‘MAENEO YAO’. “Wilaya ya Mkuranga haina ardhi kama hiyo,wilaya hii ipo karibu na jiji la dare s salaam..inapaswa kupangwa vizuri ili ilete manufaa kwa watu wa Mkuranga.
Kwa wanaotaka kuja huku (Mkuranga),nawashauri wafuate taratibu,wasivunje amani iliyopo…wanaotaka ardhi wapitie Halmashauri,wasipitie katika asasi wala kwa mtu yeyote kwa sababu taratibu za kumiliki aradhi hazielekezi hivyo,”alisema mkuu huyo.
Wednesday, August 18, 2010
Usanii kwa Wasanii????
Posted by CPWAA at 1:30 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment