SEMA NA ARTISTS!

Tuesday, August 10, 2010

Safari ya Mbeya kwenye show ya sikukuu ya Nane nane.

Tarehe 7 mwezi August nilifunga safari kuelekea mkoa wa Mbeya ambako nilikuwa nina mwaliko wa kufanya show kwenye sikukuu ya wakulima Nane nane. safari ilichelewa kidogo na tuliondoka Dar mida ya saa 6 mchana hivi. Njia nzima nililala nikaja kushtuka tuko Mo-Town, Morogoro.

Tulikuwa na gari ndogo hivyo safari ilikuwa safiii tu.

Tukatupia lunch pale karibu na Msamvu, stendi ya morogoro. Hapo nikiwa na Sister Lisa ambaye ni moja ya wawakilishi wa kampuni iliyonipa mchongo wa show hiyo Mbeya.

Kabla ya kuendelea na Safari tulipita nyumbani kwa dereva wetu pale Moro kusalimia. Kwao kuna kiwanda cha kutengenezea keki. Hizi keki tunazokula kila siku madukani na stendi kwa sh mia mia. sema sasa hapa zinatengenezwa in a special way alafu za ukweli. Hapo juu jamaa akiweka ile mix/ ingredients kwenye vikombe baaada ya kuchanganywa.

Oveni asilia ya kupikia keki.

Kitu kikiiva kinafanyiwa package, mtu mzima nikitest kiwango.....Tamu usipime.

Ujumbe.

0 comments:

Website counter